Tarime FM Online Radio ni redio ya kisasa ya mtandaoni inayorusha matangazo yake moja kwa moja kupitia intaneti. Ni jukwaa huru na la kidigitali linalolenga kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha jamii ya Tarime, mkoa wa Mara, Tanzania na Watanzania wote popote walipo duniani.
Kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya mtandao, Tarime FM imekuwa daraja linalounganisha wananchi wa ndani na wa diaspora kwa kuwafikishia habari, mijadala ya kijamii, muziki na vipindi vya moja kwa moja vinavyogusa maisha ya kila siku.
Továbbiak
Habari za uhakika – za kitaifa, kimataifa na hasa zinazohusu Tarime na mkoa wa Mara.
Elimu kwa jamii – vipindi vya siasa, afya, kilimo, biashara, mazingira na teknolojia.
Burudani – muziki wa ndani na nje, vipindi vya vijana na tamaduni.
Mijadala ya moja kwa moja (Live Talk Shows) – fursa ya wananchi kutoa maoni, kuuliza maswali na kushiriki mawazo yao.
? Tunapatikana
Kila mtu anaweza kusikiliza Tarime FM Online Radio kupitia simu janja (smartphones), kompyuta na vifaa vyote vilivyounganishwa na intaneti, popote pale duniani.